29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

Zaidi ya Vijana 1,200 wahitimu mafunzo JKT Mafinga

Na Raymond Minja, Iringa

Vijana 1,247 wamehitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kwa mujibu wa sheria ya operesheni Serekali ya Venance Mabeyo katika Kikosi cha Jeshi Mafinga JKT kilichopo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mafunzo hayo yamehitimishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendegu na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Utendaji kivita, Kanal Amosi Mollaa aliyemuwakilisha mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jen Rajabu Mabele.

Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo mkuu huyo wa RC Dendegu amewataka vijana hao kutumia mafunzo na weledi walioupata kwenye mafunzo hayo kwenda kulitumikia taifa lao .

Amesema kutokana na mafunzo waliyopata vijana hayo aliwasihi vijana hao waende kuwa wazelendo na kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wenzao huko mtaani wanakokwenda kulitumikia taifaa .

“Niwasihii sana vijana mkawe mabalozi wazuri huko muendako nendeni mkatete na kulinda nchi yenu kwani nchii hii ni yetu sote na lengo la mafunza haya ni kuanda vijana wazalendo kwa ajili ya nchi yao,” amesema Dendegu.

Aidha, aliwataka kujilinda na afya zao kwa kuepuka ngono zembe, matumiza ya madawa ya kulevya kwani wao ni nguvu kazi ya Taifa inayotegemewa Sana.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo na utendaji kivita, Kanali Amosi Mollaa alisema jukumu la jeshi ni kujenga vijana kujitegema kwa kufanya mafunzo ya nadharia na vitendo ili kwenda kujitegemea.

Kanali Mollo amewasihi vijana hao kutumia nidhamu waliyoipata kwenye mafunzo hayo ikawe salaha na tunu kwenye maisha yao ya kila siku.

“Niwasihii sana wanangu, mimi ni mzee ila nilikuwa kijana kama ninyi sasa niwasihi mkawe mfano huko muendako najuaa wengine mnaenda shule jiepusheni na migomo na maandamano yasiyo na msingi mkawe kioo cha jamii,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles