27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazindua tawi la 11 Tanga, yaombwa isaidie kuwavutia wawekezaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya NMB wiki hii imezindua rasmi tawi lake la 11 mkoani Tanga ambalo ni la 228 kwa nchi nzima ikiwa ni shehemu ya azma yake kuzisogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi.Pia uwekezaji huo ni mchango wake katika kutekeleza mpango mkakati wa taifa wa kuendeleza huduma jumuishi za kifedha nchini.

Uzinduzi wa Tawi la NMB Ngamiani lililopo Tanga mjini uliudhuliwa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba, ambao wote kwa kwa pamoja na nyakati tofauti tofauti waliiomba benki hiyo kuendelea kuchangia juhudi za kuukwamua mkoa huo hasa kwa kusaidia zaidi kuwavutia wawekezaji.

Ombi hilo iliungwa mkono na wananchi waliohudhulia hafla hiyo iliyofanyika wiki hii ambapo nao waliipongeza NMB kwa kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanga.

Wadau hao walisema ukweli wa nia njema ya benki hiyo umedhihirishwa na kufunguliwa kwa tawi hilo jipya ambalo ni la 40 katika Kanda ya Kaskazini ya NMB inayojumuisha pia mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Kwenye hotuba yake ya kulifungua rasmi tawi la Ngamiani, ambapo Mgumba, aliwahasa wananchi hasa wanaojihusisha na kilimo, uvuvi, biashara na ujasiriamali, kuzitumia vyema fursa zinazopatikana NMB hususan katika tawi lake jipya.

Alisema kufunguliwa kwake ni uthibitisho wa kukua kwa kasi kwa Tanga kiuchumi na kibiashara.

“Na ili maendeleo hayo yawe na tija na manufaa stahiki, alisisitiza kuwa yanahitaji kuchochewa na uwekezaji ambao NMB ina uwezo wa kusaidia hasa kupitia mikopo. Serikali inatambua mchango wa sekta ya fedha na hasa wa NMB katika kutoa huduma za kibenki, tunaipongeza NMB kwa jitihada za kusogeza huduma zake kwa jamii, kwani huduma hizo ni kichocheo cha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.”alisema Mgumba

Aidha, alibainisha maeneo yenye uhitaji mkubwa wa uwekezaji kuwa ni pamoja na kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ile ya kilimo cha umwagiliaji.Aliiomba NMB pia kuwakopesha wawekezaji wanaotaka kujenga maghala ya kuhifadhi mizigo na kuanzisha bandari kavu. Wahitaji wengine wakubwa wa ufadhili wa NMB ni wakulima wa katani wanaokabiliwa na upungufu mkubwa wa viwanda vya kusindika zao hilo.

“Serikali imeweka mazingira mazuri sana ya kuhakikisha jamii inafikiwa na inazitumia huduma za kibenki, nashukuru NMB imekuwa ikiunga mkono juhudi za Serikali katika hili, na hivi karibuni ilitenga Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya mikopo nafuu kwenye sekta ya kilimo,” alisema.

Akizungumza awali, Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Alfred Shao, alisema walianza na fungu la Sh bilioni 100 ambazo zilitumika kuwakopeesha wadau wa kilimo kwa riba nafuu ya asilimia 10.

Katika kuitikia wito wa serikali wa kupunguza riba hiyo, Shao alifafanua, NMB ilitenga fungu jingine la Sh bilioni 100 ambazo zinakopeshwa kwa riba ya asilimia tisa.

Aidha alibainisha kuwa pamoja na benki hiyo kuwa kinara wa kusambaza huduma za kifedha kidijitali, bado pia inaamini umuhimu wa kutumia matawi kuzipeleka karibu na wananchi.

Shao alisema ushahidi wa hilo ni kuongezeka kwa matawi 131 kutoka 97 yaliyokuwepo wakati benki hiyo inabinafsishwa mwaka 1997.

Alibainisha utayari wa NMB kuendelea kuchangia ustawi wa Tanga kwa kutoa mfano wa benki hiyo kufadhili kilimo cha muhongo na katani kwa kikwango cha juu sana. Pia NMB ni mfadhili mkubwa wa shughuli za kijamii ikitumia asilimia moja ya faida baada ya kodi kila mwaka kwa ajili hiyo.Kwenye ufunguzi wa tawi jipya, NMB ilikabidhi mabati 250 yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa Shule ya Msingi Masiwani iliyopo kwenye eneo la Ngamiani lilipo tawi hilo.

Kwa mujibu wa Meneja Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ernest Ndunguru, kufunguliwa kwa tawi la Ngamiani ni ishara ya NMB kuzingatia utekelezaji wa sera za fedha za BoT na kuhakikisha huduma za pesa zinawafikia wananchi popote walipo kwa urahisi.

“Pia ni ishara ya kukubalika kwa NMB,” kiongozi huyo wa Kanda ya Kaskazini ya Benki Kuu alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles