29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Makala| Rais Samia na dhamira ya kuleta mapinduzi makubwa Sekta ya Kilimo nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

“Ifikapo 2030 tunataka sekta ya kilimo nchini ichangie asilimia 10% ya pato la Taifa,” hii ni kaulimbiu ya wizara ya kilimo ikiwa ni agizo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika bajeti hii ya mwaka wa fedha 2022-2023 tumeshuhudia mipango na mikakati mikubwa ya kuendeleza kilimo cha kisasa katika nchi yetu ndio maana wizara ya kilimo imeweza kutenga zaidi ya Sh bilioni 900 kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini, hii imeendana sambamba na kuisimamisha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inayoongozwa, Raymond Mndolwa na kukabidhiwa bajeti ya Sh bilioni 361 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru.

Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Maonyesho ya 88 / 2022. (Aliyevaa Kofia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Kushoto kwa Rais ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa.

Hii ni baadhi ya mikakati na mipango ambayo inaonesha dhahiri bayana kwamba Rais Samia Suluhu kupitia wizara ya kilimo ameamua kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo kupitia tume ya umwagiliaji taifa.

“Kwanza ni utiaji saini wa mikataba 21 ya Wizara ya Kilimo yenye thamani ya Sh bilioni 182 sawa na asilimia 52 ya bajeti ya tume ya umwagiliwaji, ambao pia ulishuhudiwa na Rais Samia Agosti 8, mwaka huu.

“Kilimo ni Sayansi, na sayansi ni utafiti, hivyo Mhe.Rais ameona tija katika kufanya utafiti katika sekta ya kilimo hivyo ameongeza fedha ya utafiti kutoka Sh bilioni 7.35 hadi Sh bilioni 11.6 kwa ajili ya utafiti wa mazao, mbolea, ardhi yenye rutuba na nyanja nyingine.

“Sambamba na hayo ifikapo mwaka 2025, Mhe Rais anataka vijana wasio pungua millioni 1 wajiajiri katika mnyororo wa kilimo, hivyo kufikia malengo hayo, kupitia wizara imeandaa programu iitwayo BUILDING TODAY FOR BETTER TOMORROW kwa ajili ya ujenzi wa mashamba makubwa (Block Farming) kwajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa  vijana, Mfano Dodoma kuna ekari 11 zinazoandaliwa, Mbeya ekari 41, Njombe ekari 23,144 ikiwa ni sambamba na utengaji wa fedha takribani Sh bilioni 150 ambazo zitasaidia wakulima ikiwa ni pamoja na kushusha bei ya mbolea kwa zaidi ya asilimia 50,” anasema Mndolwa.

Aidha, Mndolwa anaendelea kufafanua kuwa, Rais Samia kupitia wizara ya kilimo imeweza kununua pikipiki zaidi ya elfu 7,000 kwa ajili wa Mabwana Shamba na maofisa Ugani ambao watakuwa wanapitia mashambani kufanya ukaguzi wa mashamba, upimaji wa ardhi zenye rutuba na ukaguzi wa mazao.

“Serikali imeweza kuongeza bajeti ya huduma za ugani kutoka Sh bilioni 17.7 hadi Sh bilioni 51.45, kuongeza fedha za uzalishaji wa mbegu kutoka Sh bilioni 5.42 hadi Sh bilioni 10.58, sambamba na kuongeza bajeti hiyo, Rais Samia amewezesha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency – NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cerial and Other Produce Board – CPB) kwa jumla ya Sh bilioni 129 ili waweze kuongeza ufanisi.

“Kupitia tume ya umwagiliaji imejipanga kufufua miradi ya kilimo 33, ujenzi wa mabwawa 13 na mabonde 22 ya maji na visima nchi nzima vyenye dhamani ya Sh bilioni 58, hii itasaidia upatikanaji wa maji kila muda kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea kilimo cha msimu.

“Kwani kam atunavyoamini na kutambua kuwa kwasasa kilimo cha umwagiliaji ni mwarobaini kwa kilimo mvua hivyo tume imejipanga kuongeza usimamizi wa kilimo hiki nchi nzima ikiwamo kujenga na kufungua ofisi zake 146 kila Wilaya nchini na nyingine 17 kila Mkoa.

“Pia Vyama vya Ushirika vimekuwa chachu ya wananchi kupata huduma za kijamii ambapo kwasasa vimeanza kutoa huduma ya bima ya afya kwa wanachama wake kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (National Health Insurance Fund-NHIF) na mabenki. Mkakati umewekwa kati ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na NHIF kuhakikisha wanachama wa Vyama vya Ushirika wanapata huduma ya afya ya uhakika na kwa wakati.

“Hadi Aprili, 2022 wanachama zaidi ya 1,000,000 walikuwa wamejiunga kwenye mpango huo, serikali ya Awamu ya Sita imeongeza fedha za ununuzi wa nafaka kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency – NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cerial and Other Produce Board – CPB) kutoka Sh bilioni 19 mwaka 2020/2021 hadi Sh bilioni 119 mwaka 2021/2022 Hadi Aprili, 2022 fedha hizo zimewezesha ununuzi wa tani 183,045.384 za mahindi, mpunga na mtama. Hatua hiyo, itaiwezesha nchi kuwa na uhakika wa chakula na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” anasema Mndolwa na kuongeza kuwa:

“Kuonesha mfano kwamba haya yote yanawezekana Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ikishirikiana na chama cha Ushirika wa AMCOS, CHABUMA kikiongozwa na mwenyekiti wake Ndg. David Mwaka wameweza kuanda shamba la Block Farming lenye hekari 300 kwajili ya ulimaji wa zao la zabibu ambalo ndio nembo ya Mkoa wa Dodoma, na inasemekana zabibu inayolimwa Dodoma inauwezo wa kuzaa Mara mbili kwa mwaka wakati Zabibu yingine duniani huzaa mara moja kwa Msimu, na kumekuwa na mwamko mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo la Chinangali wilaya ya Chamwino kujiunga na kilimo hicho kwami wameanza kuona tija na Nia ya serikali kwa wananchi wake.

“Watanzania hasa vijana inabidi tubadilishe mtazamo na tuchangamkie hii fursa ya kilimo, kuna shairi la zamani linasema UKITAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI Vijana tuache Mtazamo wa kutaka kazi rahisi kupata matokeo haraka kwani haidumu bali tuchague kilimo kinachoweza kutajilisha Watanzania wengi kwa pamoja,” anasema Mndolwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles