30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Zahera: Hali ngumu ya wachezaji ndiyo iliyoniliza jana

Lulu Ringo, Dar es Salaam.


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kilichomtoa machozi jana Decemba 3 alipokuwa akihojiwa baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Tanzania Prisons, ni baada ya kukumbuka hali ngumu ya kiuchumi wanayopitia wachezaji wake lakini wanajitoa kwa moyo na kupata ushindi.

Baada ya kuangua kilio hicho mashabiki na wadau mbalimbali wametoa maoni tofauti kwenye mitandao ya kijamii wengine wakisema kilio kile kilitokana na kutokukubaliana na maamuzi ya  mwamuzi wa kati, huku wengine wakisema kilitokana na furaha na mapenzi aliyonayo kwa Yanga.

Lakini Mtanzania Digital leo Decemba 4 imezungumza na Zahera kuhusiana na kilio hicho amesema, wachezaji wake wana hali ngumu ya kiuchumi lakini hawakati tamaa kila siku wanazidi kupambana kwa ajili ya timu yao bila kuchoka wala kurudi nyuma.

“Nimejikuta natokwa machozi nilipokumbuka magumu waliyonayo wachezaji wangu, jinsi wanavyopambana, wanavyojitolea na furaha waliyopata mashabiki pale uwanjani baada ya ushindi, nikajikuta natokwa na machozi,” amesema Zahera.

Katika mchezo huo, Tanzania Prisons ilikua ya kwanza kupata goli la kuongoza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Jumanne Elifadhili dakika ya 45, goli lililodumu hadi dakika ya 76 ambapo Ibrahim Ajib aliposawazisha Yanga kwa pia kwa mkwaju wa penalti.

Baada ya goli hilo kurudi mchezo ulibadilika ukawa wa kushambuliana kwa kasi lakini mabadiliko aliyoyafanya kocha Mwinyi Zahera ya kumuingiza, Hamisi Tambwe yaliitoa yanga kifua mbele baada ya mchezaji huyo kufunga magoli mawili dakika ya 85 na 90 na kufanya mchezo umalizike kwa Yanga kushinda mabao matatu kwa moja.

Kwa sasa Yanga Sc inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na jumla ya alama 38, imecheza michezo 14, imeshinda 12 na kutoa sare miwili.

 

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles