ZAA ipo tayari kimataifa

0
648

Na VICTORIA GODFREY-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAA), umesema upo tayari  kushiriki mashindano  mbalimbali ya kimataifa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Katibu Mkuu wa ZAA, Yassin Muhidini alisemaushiriki wao ni  katika riadha ya mbio fupi.

Alisema kuwa, mpango wa ZAA ni kuhakikisha inapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kusaka viwango vya kufuzu michezo ya Olimpiki ijayo.

“Malengo yetu tunataka kuhakikisha kila mashindano ya kusaka viwango yatakavyotakangazwa katika nchi mbalimbali,  tutakuwa tunapeleka  ili washiriki kikamilifu  na kupata nafasi  ya kushiriki michezo ya Olimpiki.

“Zanzibar tunajivunia sana kuwa na wanariadha wazuri wanaoshiriki mbio fupi kutokana na asili ya mbio hizi ni huku, hivyo tunayo mipango ambayo tunatumia fursa ya kipindi hiki cha janga la corona ili tuweze kutimiza malengo yetu,”alisema Muhidini.

Alisema ili kufikia malengo hayo,  wanariadha wenyewe  wanatakiwa kujituma kwa bidii kufanya  mazoezi yao  binafsi  kwa  kufuata  program  za mazoezi  wanazopewa na makocha wao .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here