27.5 C
Dar es Salaam
Friday, July 1, 2022

Mashindano ya kickboxing ya vijana yaja

Na VICTORIA GODFREY-DAR ES SALAAM

MCHEZA Kickboxing maarufu nchini, Japhat Kaseba amesema kuwa, ana mpango wa kuandaa mashindano ya vijana ya mchezo huo, ambayo itafanyika baada ya tamko la Serikali la kuruhusu mikusanyiko ya watu, ikiwamo michezo.

Machi 17 mwaka huu, Serikali ilipiga marufuku  mikusanyiko ya watu, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vya corona.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaseba alisema  lengo  ni  kuchagua timu ya vijana ambayo itaandaliwa kwa shiriki mashidano ya kimataifa.

“Tayari vijana wapo kutoka mikoa mbalimbali ambao watapata fursa  ya kushiriki mashindano hayo,”alisema.

Kaseba alisema kuwa, mpango uliopo ni kuendelea kuhamasisha vijana wengi waweze kujitokeza kujifunza mchezo huo, kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa, matarajio yao kuona Tanzania inakuwa na nyota wengi ambao wataitangaza vyema Tanzania.

“Ninatamani sana kuona vijana wanafuata nyayo zangu na kupata warithi wengi zaidi,”alisema Kaseba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,419FollowersFollow
544,000SubscribersSubscribe

Latest Articles