23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

YARA yawahakikishia wakulima upatikanaji mbolea

Na Mwandishi wetu-Dar es salaam

KAMPUNI ya Mbolea ya YARA Tanzania imewahakikishia wakulima kupata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati na bei inayokubalika sokoni  sambamba na msimu wa kilimo ili kuleta tija na kuongeza uzalishaji wa mazao hapa nchini.

Akizungumza na Mawakala na wasambazaji wa mbolea kutoka kanda zote nchini, Mkurugenzi  wa YARA Tanzania, Winstone Odhiambo alisema upatikanaji wa mbolea kwa wakati na bei nzuri kwa mkulima ni moja ya vipaumbele vya kampuni yake kuona uzalishaji wa mazao unaongezeka.  

“YARA inaishukuru serikali kwa kuunga mkono juhudi  zetu za kukuza na kuendeleza kilimo hapa nchini. Kama kampuni tumejipanga kuhakikisha mkulima anapata mbolea kwa wakati na matumizi bora ili kuleta tija katika uzalishaji,” alisema Odhiambo.

Alisema kampuni imeshatoa elimu kwa mawakala na wasambazaji wote nchi nzima umuhimu wa kumfikishia mbolea mkulima kwa wakati na wakati huo maofisa ugani wamekuwa wakitoa mafunzo ya matumizi bora ya mbolea kwa wakulima.

Alisema YARA imejipanga vizuri katika msimu unaokuja wa kilimo kwa kuhakikisha mbolea inakuwepo wakati wote na mawakala na wasambazaji wanawajibika katika kuwafikishia huduma wakulima ya namna bora ya matumizi ya mbolea ili tija ya uzalishaji iweze kuongezeka.

“Wakati tuelekea kuanza msimu wa kilimo mwezi ujao, tumetoa elimu kwa mawakala wetu na wasambazaji kabla hawajaanza kuuza mbolea kwa wakulima. Elimu kwanza ni muhimu sana katika kufanikisha kilimo bora na chenye tija,” alisema Odhiambo.

Odhiambo alisema kuwa mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa kuwakutanisha mawakala na wasambazaji wa mbolea ya YARA ulilenga pia kukusanya maoni, ushauri na changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao ili kuyatafutia ufumbuzi kabla msimu haujaanza.

“Mbali ya kujiandaa na msimu wa kilimo 2019/20, katika mkutano huu tumeweza kutoa bonasi kwa mawakala waliofikia malengo ya kampuni katika usambazaji mbolea na kuwahamasisha wengine kujituma zaidi katika usambazaji  na mfaidisha mkulima,” alisema.

Alisema lengo la kampuni ya YARA pamoja na kufanya bisahara lakini wamejikita zaidi katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa kupima afya ya udongo kabla ya kufanya kilimo hali itakayompa majibu ya zao gani apande, mbolea gani anapaswa kutumia na kwa kiwango gani kulingana na hali ya udongo wake hali itakayoonge kwa tija na uzalishaji wa mazao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles