TAEC: Watanzania njooni Nanenane mjifunze teknolojia ya nyuklia

0
960
Timu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC), katika picha ya pamoja kwenye banda lao lilipo katika uwanja wa Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo wanatoa elimu kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo namna ya teknolojia ya nyuklia inavyotumika katika sekta ya Kilimo,Maji na Mifugo na Mazingira na namna ya inavyosimamia na kuthibiti matumizi salama ya mionzi.

Mwandishi Wetu, Simiyu

Wananchi wanaoishi mikoa ya Kanda ya Ziwa na mikoa jirani, wametakiwa kuhudhuria kwa wingi kwenye banda lao katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa yanayofanyika katika Uwanja wa Nyakibindi, mkoani Simiyu ili kujipatia elimu ya namna ambavyo teknolojia ya nyuklia inavyotumika katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo kilimo, mifugo, maji na afya.

Akizungumza katika banda la tume hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Utafiti wa TAEC,  Yesaya Sungita amesema wananchi watapata elimu ambayo itawawezesha kupata uelewa juu ya masuala ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na udhibiti wake hapa nchi ili kutoleta madhara kwa wananchi na mazingira.

“TAEC imekuwa ikihakikisha teknolojia ya nyuklia inatumika ipasavyo katika sekta muhimu kama vile maji, mifugo na kilimo.

“Lakini mbali na wananchi kujua kuhusiana na teknolojia hiyo ya nyuklia, pia wataweza kufahamua namna TAEC inavyofanya kazi ya kusimamia na kuthibiti matumizi salama ya mionzi nchini,” amesema Sungita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here