25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Yanga, Simba wamlilia Mzee Akilimali

NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetuma salaam za pole kwa aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, marehemu Mzee Ibrahim Omary Akilimali.

Mzee Akilimali alifariki dunia jana asubuhi akiwa katika hospitali ya Bagamoyo,Pwani ambapo alikua akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu sasa.

Alipata kadi yake ya kwanza ya uanachama wa Yanga mwaka 1972 na amewahi kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo kabla ya uteuzi wake katika Baraza la Wazee la klabu. 

Akilimali ambaye pia alikuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atakumbukwa kwa misimamo yake zaidi ya kuitetea Yanga isimame kama ilivyo na si kuchukuliwa na watu huku akipendekeza zaidi mfumo wa hisa.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa afisa habari wake Hassan Bumbuli, ilisema wamepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa kiongozi huyo ambaye alikua na mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo.

“Klabu ya Yanga inasikitika kutangaza kifo cha mwanachama wao na wamepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa kutokana na mchango wake mkubwa nani ya timu hiyo”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa upande wa aliyekua mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Simba, Mzee Hamis Kilomoni alisema kama wadau wa soka wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubw akwnai Akilimali alikua ni zaidi ya rafiki kwake licha ya uhasimu wao katika klabu wanazoshabikia.

Msiba huo kwa sasa umehamia nyumbani kwake Tandale kwa Mtogole na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni katika makaburi ya Mtogole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles