25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Kili Stars yapenya nusu fainali, Zanzibar ikiaga Cecafa

NA JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

TIMU ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ ,  jana ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Chalenji ya  nchi za Afrika Mshariki na Kati (Cecafa) inayoendelea nchini Uganda, licha ya kutoka suluhu na Sudan.

Kwa matokeo hayo Tanzania Bara, inaungana na Kenya kutinga hatua hatua zikitokea Kundi B.

Katika pambano hilo gumu, Stars na Sudan zilishambuliana kwa zamu, lakini hadi dakika tisini zinakamilika hakuna upande uliofanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake.

Stars imekamilisha hatua ya makundi kwa kumaliza nafasi ya pili kweye msimamo wa Kundi B, ikikusanya pointi nne ilizozipata kupitia michezo yake michezo ikilazwa bao 1-0 na Kenya, ikainyuka Zanzibar bao 1-0 kabla ya suluhu na Sudan.

Kenya imemaliza vinara wa kundi hilo ikikusanya pointi tisa, ilizozipata baada ya kuinyuka Kilimanjari bao 1-0, ikaitunguia Sudan mabao 2-1 kabla ya kuikandamiza Zanzibar bao 1-0.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa Kilimanjaro, Juma Mgunda alisema vijana wake wamepambana kwa hali zote na walipania kupata matokeo mazuri lakini wanashukuru kufanikiwa kuingia hatua nyingine.

“Mchezo ulikua na upinzani mkali, Sudan ni wazuri lakini vijana walipambana kwa hali zote ili wapate ushindi ingawa haikuwa hivyo, kwa sasa tunajipanga kwa hatua inayokuja ili tuwezwe kufanya vizuri na kufika hatua ya fainali,”alisema Mgunda.

Alisema baada ya kufanikiwa kufuzu nusu fainali, wanajipanga upya ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kutinga nusu fainali.

“Tumefanikiwa kutinga nusu fainali, ni hatua nyingine ambayo lazima uwe na mikakati tofauti na ile ya hatua ya makundi kwakua huko ukipoteza mchezo na safari yako imewadia.

“Tunatakiwa kucheza hatua hiyo kwa staili nyingine, vijana wanafahamu hilo sina  shaka watapambana kuhakikisha tunavuna,”alisema  Mgunda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles