Salah azidi kuipaisha Liverpool

0
1130

LIVERPOOL, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohammed Salah jana alifunga mabao mawili yaliyoiwezesha timu yake ya Liverpool kuibuka ushindi wa mabao 2-0 dhidi Watford katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield,jijini  Liverpool.

Salah alifunga mabao hayo dakika za 38 na 90 na kuifanya Liverpool kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo.

Ushindi huo  yanaifanya Liver kuzidi kujikita killeleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza michezo 17, ikishinda 16 na kutoika sare mmoja.

Liverpool sasa imefanya pengo la pointi kati yake na mabingwa watetezi, Manchester City kufikia 17, hata hivyo City ina mchezo mmoja mkononi ambao itacheza dhidi ya Arsenal leo.

Majogoo hao wa jiji la Liverpool, waliuanza mchezo huo kwa kasi na kulisakama lango la Watford kama nyuki kupitia mashambulizxi ya mipira mirefu na pasi za haraka haraka.

Dakika 38, Salah aliindika Liver bao la kwanza nakuifanya timu kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Liverpool  ilikuja juu zaidi ikilenga kupata mabao yatakayowawezesha kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo.

Hata hivyo uimara wa safu ya ulinzi ya Watford ulikuwa kikwazo vijana hao wa Jurgen Klopp kupata mabao zaidi.

Dakika ya 90, Salah alipigilia msumari wa pili na kuifanya Liverpool kujihakikishia pointi tatu katika mchezo huo.

Hadi dakika 90 za mtanange huo zinakamilika Liverpool  iliondoka uwanjai na pointi tatu na mabao mabao 2-0 dhidi ya Watford.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here