24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga itambue ina kazi kubwa 2021\2022

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

YANGA ni kati ya timu zilizofanya usajili wa wachezaji wengi katika kipindi hiki kuboresha  kikosi chake kuelekea msimu wa 2021\2022.

Usajili huo umezingatia upungufu ulioonekana  msimu uliopita  ambapo imeshindwa kuchukua ubingwa wamashindano yote, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

Hali hiyo iliwanyong’onyesha mashabiki wake ambao waliaminishwa kuwa watachukua ubingwakatika msimu huo kutokana na usajili waliofanya lakini matokeo yake mambo yakaenda tofauti.

Ukiangalia katika msimu uliopita Yanga ilifanya  usajili wa wachezaji wengi tena waliotua kwa mbwembwe zote na kufanyiwa mapokezi makubwa na mshabiki.

Kuelekea msimu mpya Wananchi hao wamefanya tena kufuru ya usajili na kuachana na baadhi ya nyota wake ikiwamo makipa wawili waliokuwa waliokuwa tegemeo kikosini, Metacha Mnata na Farouk Shikalo.

Katika maboresho ya msimu mpya  mbao wanajangwani hao watashiriki   Ligi ya Mabingwa Afrika kuna maingizo mapya  zaidi ya 10.

Wachezaji hao ni Yusuph Athuman,Fiston Mayele,Heritier Makambo, Shaban Djuma Djigui Diarra,Khaleed Aucho,Eric Johora, Dickson Ambundo,David Bryson,Jesus Moloko na Yannick Bangala.

Usajili huo ni mzuri kulingana na historia ya wachezaji hao  kwa kilewalichokifanya katika timu wanazotoka, huku  Makambo akiaminiwa zaidi kufanya vizuri kutokana na rekodi yake Jangwani.

Pamoja na yote hayo, uongozi wa Yanga unatakakiwa kutambua kuwa bado haujamaliza kazi, hasa ukizingatia inakabiliwa na  michuano ya kimataifa.

 Ni vizuri  Wanangwani hao wakatazama nyuma na kuweka mikakati mipya ya kuingia katika msimu mpya kwa sababu kusajili  pekee hakuwezi kuifanya timu  bora.

Yapo mambo mengi yanahitajika ili kukifanya kikosi kiwe bora na ushindani ikiwamo kuweka msingi  na malengo  kwa kufanya vitendo na si maneno.

Ikumbukwe msimu uliopita kulikuwana mamneno mengi ya kuwaamninisha wadau kuwa Yanga ni bora, imefanya usajili hivyo ubingwa ni lazima.

Kama  Yanga inataka kufanya vizuri Kimataifa na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, basi  uongozi ujipange  zaidi, hata kwa kuangalia watani zao walifanya nini hadi kufanikiwa kufika robo fainali mara mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Uongozi utambue kuwakwa sasa mashabiki wao wanahitaji makombe na kufanya vizuri Kimatiafa na si maneno bali vitendo.

Katika kutambua kuwa Wanajangwani hao wana deni na kiu ya wadau wao kuona kikosi bora, ni umati uliojitokeza jana katika kilele cha Wiki ya Wananchi na maoni mbalimbali waliyotoa.

Ili kulinda rasilimali hiyo ya watu kama kauli mbiu inavyosema kuwa ‘Sisi tuna Watu’, lazima iambatane na matokeo  mazuri uwanjani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles