24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Viwanda yanadi fursa za uwekezaji kwa wawekezaji wa Kichina

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wizara ya Viwanda na Biashara imefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka nchini China na kuwaonyesha fursa zinazopatikana ili waweze kuwekeza nchini ili ziweze kuchochea uwekezaji, ajira na kuongeza Pato la Taifa.

Akizungumza Machi 27 jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo hayo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sempeho Manongi amesema wamepata wageni kutoka nchini China katika Jimbo la Changzho ambao wamekuja kwa ajili ya kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuleta ushirikiano.

Amesema wawekezaji hao wameletwa kwa kushirikiana na kampuni mbili ambazo ni kampuni ya Canopus Energy Solutions na Amec Group katika wangeni hao wameambatana na viongozi wa serikali na wawekezaji na timu ya wataalam.

“Tumewaonyesha fursa zilizopo za viwanda na maeneo ya uwekezaji katika sekta zote muhimu kwa nchi yetu ili waweze kuimarisha uchumi wa nchi.Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo maalumu,” amesema Manongi.

Ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana na baadhi ya maeneo hayo hivyo wakitoka hapo wanaelekea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwenda kupata taarifa ya kina kwenye masuala ya uwekezaji ili waweze kuingia makubaliano kwenye maeneo ambayo wameona ambayo yanahitajika kwaajili ya uwekezaji.

Manongi amesema wao wameonyesha maeneo ya sekta ya kilimo katika kuongeza mazao ya kilimo maeneo ya uzalishaji wa madini ya viwanda ambayo ni muhimu mfano chuma

Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo maalumu.

Ameongeza kuwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wana maeneo makubwa ambayo wanaweza kuwekeza uwekezaji ikiwemo Kilimanjaro machine tools, Tange lipo Tanga, Kibaha maeneo kwa ajili ya uwekezaji.

Amesema wameshauriana kuna uwekezaji wa moja kwa moja, wa ubia na kubadilisha ujuzi na uzoefu ambao utaletwa nchini.

Aidha, amesema katika miradi saba ikitekelezwa kuzalisha MEGAWATI
zaidi ya 1400 wanahitaji umeme kwa wingi hivyo wakipata uwekezaji kikubwa kupata utalaamu wa hiyo sekta ndio wanahitaji kwa wingi na baadae wawekezaji wakijitokeza watapata umeme kwa wingi na uzalishaji utaongezeka ajira na matumizi ya umeme.

Naye Kiongozi wa Ujumbe kutoka Serikalini ya Jimbo la Changzho, Shen Don amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja mbalimbali wanahitaji kuwekeza katika uzalishaji katika viwanda.

Kwa upande wake, Mhandisi Anna Nyangasi wa Kampuni ya Canopus Energy Solutions amesema kampuni yao inajihusisha na uuzaji wa dhana za kilimo, usafirishaji na uzaji usambazaji bidhaa za solar.

Kupitia Kampuni mbili hizo wameaandaa uwekezaji maeneo yafuatayo pamoja na kilimo, afya, vifaa vya ujenzi, vifaa vya uchakataji

“Watawekeza katika maeneo mashine za kilimo watawekeza dola za kimarekani milioni 24.5, vifaa vya hospitali watawekeza dola za kimarekani milioni 6.

“Vifaa vya umeme watawekeza dola za Kimarekani milioni mbili vifaa vya ujenzi dola za kimarekani milioni 11.3 vifaa vya uchakataji wa mafuta dola za kimarekani milioni 43,”amesema Mhandisi Anna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles