22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Wizara ya Afya yabaini ubadhilifu wa Sh milioni 520 za NHIF Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebaini ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 520 za mfuko wa bima ya afya NHIF katika hospitali za rufaa za wilaya na maduka ya dawa ya taasisi binafsi mkoani Kilimanjaro.

Miongoni mwa hospitali hizo ni hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazi (KCMC) Sh million 245, hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro Mawnzi Sh milioni 38, hospitali ya St Joseph Sh millioni 46, hospitali ya Huruma Rombo Sh millioni 900,000, hospitali ya Usangi Mwanga Sh milioni 1,156,000, Moshi Haelth Center Sh 480,000.

Aidha, maduka ya dawa za taasisi binafsi ni Kibo Phamcy Sh millioni 33, Mount Kibo Phamcy Sh molioni 50, Kilimani Juu Pharmacy Sh milioni 36, ACDA Pharmacy Sh milioni 33, Msafiri Phamcy Sh milioni 55, RNA Sh milioni 2, pamoja watumishi sita Sh milioni 8,429,000.

Niabu Waziri ya Afya, Dk. Godwin Mollel amebainisha hayo leo Jumatatu Julai 12, 2021 mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake mkoani humo ambapo amesema serikali haipo tayari kulifumbia macho ubadhilifu fedha wa fedha za mfuko wa bima ya afya NHIF.

Dk. Mollel amesema watumishi katika hospitali wasiokuwa waminifu wanacheza na mfumo kwa kushirikiana na maduka ya dawa wanaandikia mgonjwa dawa inaonekana ametumia badala yake wanawapa madaktari na manesi wanakwenda kutumia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai amesema vyombo vya usalama imeshachukua hatua za haraka kwa ili fedha hizo zirejeshwe na watumishi waliohusika na ubadhilifu huo kuchukuliwa hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles