Wezi wa vifaa vya kujingika na corona wapewa onyo

0
988
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela

Amina Omari, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela amewaonya  watu wanaohujumu  juhudi zinazofanywa  na wadau mbalimbali waliojitolea kutoa msaada wa vifaa kinga kwaajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababisha virusi vya corona kwa kuiba vifaa hivyo zikiwemo ndoo na koki za maji.

Ametoakauli hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi katika kituo cha daladala cha  Ngamiani wakati akipokea msaada wa  matenki ya maji  yaliyotolewa na wadau mbalimbali.

“Hivi karibuni kumeibuka wizi wa vifaa kinga kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo stendi za mabasi  watu wanaiba ndoo na koki Hali inayofanya watu wengine wapate adha.

 “Kuiba vitakasa mikono ni kujiangamiza mwenyewe na watu wengine, naomba niwape onyo watu hawa waache tabia hii na tukiwakamata tutawachukulia hatua ” amesema RC Shigela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here