23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Mafuriko yasomba zaidi ya nyumba 20 Kilimanjaro

Upendo Mosha,Moshi

Zaidi ya nyumba 20 na daraja moja zimesombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha mkoani Kilimanjaro na kusababisha mafuriko katika mto Rau uliopo Manispaa ya Moshi.

Mvua hizo zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Jumanne Aprili 21, zimeshabisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, maji na umeme na kupelekea kuathiri mawasiliano ya maeneo hayo.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa huo, Anna Mgwhira wakati alipotembelea maeneo hayo amesema mvua hizo zimeleta madhara makubwa hasa kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mto huo.

“Mvua hizi zimeleta madhara makubwa kwa wananchi waishio pembezoni mwa mto huum mpaka sasa ni nyumba nyingi zimechukuliwa na maji lakini pia kuna watu watano wamejeruhiwa na mmoja anasemeka amechukuliwa na maji, “amesema RC Mgwhira.

Ameongeza kuwa taarifa zaidi ya adhari za tukio hilo zitatolewa baada ya kupokea taarifa kutoka Chama cha msalaba mwekundu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles