Papa Fololo aiweka wazi ‘Hakupendi’

0
941

Quebec,Canada

MWANAMUZIKI mwenye asili ya Tanzania anayeishi Brossard, Quebec nchini Canada, Papa Fololo, amewaomba wapenzi wa muziki mzuri kuipokea video ya wimbo wake mpya, Hakupendi aliyomshirikisha prodyuza Fraga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Papa Fololo alisema anaamini mashabiki zake wengi wapo Afrika Mashariki hasa Tanzania hivyo anahitaji sapoti yao.

“Ni wimbo wa mapenzi ambao nimezungumzia hali halisi za mahusiano mengi. Mapenzi ya kweli yamepungua, wengi wanadanganya ndio maana nimeona nije na ngoma hii ambayo video yake imeongozwa na Brown Fx na sasa ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema Papa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here