23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Silaa atoa miezi sita kwa wataalamu wa ardhi nchini kutoa elimu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewataka wataalamu wa ardhi nchini kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa vijiji taratibu za upangaji na upimaji wa ardhi.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo leo Desemba 11, 2023 wilayani Musoma Mkoa wa Mara wakati akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Vijiji 975 nchini.

Waziri Silaa amewapa muda huo wa miezi sita (6) wataalamu wa ardhi katika wilaya zao nchi nzima ili kuhakikisha wanawafundisha wananchi na viongozi wa vijiji maana ya upangaji na upimaji wa viwanja na kuwapa uelewa ili kuepuka upangaji holela wa vijiji.

Amesema kazi hiyo haihitaji gharama kwani ni suala la elimu ambalo linaruhusiwa kutolewa katika mikutano ya wenyeviti wa vijiji na kuwaelekeza maana ya upimaji wa awali wa viwanja na mashamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles