26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania eneo linalopendekezwa zaidi kibiashara

Na Mwandishi wetu

Tanzania imetengeneza nafasi muhimu katika biashara Afrika kutokana na uhusiano  na mataifa mengi ulimwenguni, hivyo kuwa na uwezo wa kupata nafasi ya uwanzilishi  wa ukuaji wa viwanda na kuhakikisha fursa hiyo inakua.

Akizungumza jana Desemba 10, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya   EnergyNet, Simon Gosling amesema Tanzania ni eneo muhimu kwa shughuli  za uwekezaji barani, ambapo inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano  wa tano wa mwaka wa kimataifa  wa Tanzania Energy Cooperation  Summit( TECS) unatarajia  kufanyaia Januari 31 hadi Februari  mwaka 2024 jijini Arusha.

“Kwa kuzingatia nafasi ya Tanzania kama mhimili wa nishati kikanda, mada zitakazojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na mtazamo wa kiuchumi  wa Tanzania na uwezo wa maendeleo ya nishati  pamoja na kupanga njia bora ya kujenga soko la umeme kikanda,” amesema Gosling.

Mkutano wa TECS Januari, 2023.

Amesema kuona ukuaji  wa pato la taifa kwa asilimia 6 ifikapo mwaka 2025, huku ikishudia mamilioni ya uwekezaji wa dola unaolenga kuwekeza kwenye miundombinu,  maji, umeme na gesi asilia (LNG) na miradi ya nishati ya jua kati ya miaka ya hivi karibuni.

Amesema ni Taifa lililotwajwa kwa eneo lake la kimkakati mashariki mwa barani  Afrika kwa wingi wa maliasili  na ongezeko la uwekezaji hivi karibuni  katika sekta ya nishati.

Amesema mkutano huo wa  wa TECS24 umeratibiwa na Energy Net hautoainisha mafanikio  hayo ya kujivunia  pekee bali itaangazia fursa zijazo za biashara na miradi ya uzalishaji  inayotarajia kubadilisha nchi na ukanda huo zaidi.

Ameeleza changamoto zinazohusiana na fedha na dhamana pia zitajadiliwa ili kuchochea ari zaidi ya majadiliano na kuhakikisha  sekta ya umeme nchini inaendelea  kuimarika zaidi.

“Ushirikiano wa sekta za umma na binafsi  katika  miradi ya usafirishaji  pia utakuwa kwenye ajenda pamoja na wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha  utawala na kanuni na nafasi muhimu ya nishati mbadala na washiriki  watapewa fursa  ya kutoa mawazo na kuweka mifumo  imara zaidi katika biashara na uwekezaji, “amesema.

Aidha Gosling  amesema wawekezaji kutoka sekta  mbalimbali za fedha na serikali zitakutana kuonyesha uwezo mkutano  huo.

Naye Mkuu Mwenza wa ‘Infrastructure Sector Group Afrika’, Aleem Tharani amesema mkutano huo wa tano wa kimataifa  wa Tanzania Energy Cooperation Summit unaweka alama muhimu  kwa sekta ya nishati barani Afrika.

“Kwa kuwaunganisha wawekezaji, taasisi za serikali na watalaamu wa sekta, tunachochea majadiliano muhimu kwa ajili ya kukuza ramani  ya nishati ya Tanzania, kutoa kipaombele kwa gesi na nishati mbadala na kuboresha usafirishaji wa kikanda, ” amesema  Tharani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles