22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AITAKA MAMCU KUJITAZAMA UPYA

Na Florence Sanawa, Mtwara

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mrajisi wa Ushirika Dk. Titto Haule kuangalia kwa umakini utendaji na ufanisi wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Mtwara (MAMCU) na viongozi wote ili kubaini kama wanakidhi makusudio yake.

Aidha, ameagiza ikiwezekana chama hicho kivunjwe ili vianzishwe vyama kilele viwili vitakavyoweza kuhudumia wakulima katika maeneo yao ili kuongeza tija.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumanne, Februari 27, wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Chiungutwa wilayani Masasi, mkoani hapa.

“Napata mashaka kuhusu uwezo wao wa kuwahudumia wakulima, hivyo naagiza kuharakishwa kwa utekelezaji wa agizo hilo ili kurahisisha utoaji wa huduma,” amesema Waziri Mkuu.

Amesema kwa mujibu wa takwimu zilizopo, haamini kama chama hicho kina uwezo wa kuhudumia maeneo yaliyokusudiwa, hivyo kusababisha wakulima kutofikiwa kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza wakulima wa korosho kujiwekea akiba ya fedha ili ziweze kuwasaidia katika ununuzi wa pembejeo.

“Mwaka huu Serikali haitagawa pembejeo ya salfa kwa sababu mwaka jana iligawa bure ili kuwahamasisha wakulima kufufua zao hilo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu amewataka wakulima wa korosho kupanda miche mipya ya mikorosho na kuiondoa mikorosho ya zamani iliyozeeka ili waweze kuzalisha mazao bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles