23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

KOREA KUSINI YAITAKA MAREKANI IPUNGUZE MASHARTI MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI

SEOUL, KOREA KUSINI


RAIS wa Korea Kusini, Moon Jae-In, amesema Marekani inapaswa kupunguza masharti kuwezesha mazungumzo kati yake na Korea Kaskazini.

Kadhalika amesema Korea Kaskazini pia inapaswa kuonyesha nia ya kuachana na mipango yake ya nyuklia.

Katika mkutano wake na Naibu Waziri Mkuu wa China, Liu Yandong mjini hapa, Moon alisema katika siku za hivi karibuni, Korea Kaskazini imeonyesha utayari kufanya mazungumzo na Marekani.

Marekani nayo pia inazungumzia umuhimu wa mazungumzo na Korea Kaskazini.

Moon alisisitiza ni muhimu kwa Marekani na Korea Kaskazini kukaa katika meza ya mazungumzo ya pamoja haraka.

Awali juzi Korea Kaskazini, kupitia afisa wake wa kijeshi, Jenerali Kim Yong Chol, ilisema iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani.

Marekani na Korea Kaskazini hazijawa na uhusiano mzuri kutokana na mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini hatua ambayo imeifanya Marekani kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vikali zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles