23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu aipa kazi maalum Bodi ya Korosho

NA MWANDISHI WETU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Bodi ya Korosho Tanzania, ihakikishe inatafuta masoko ya uhakika yenye bei nzuri na kuwanufaisha wakulima.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo jana Julai 22,2021, wakati akizungumza na wakuu wa mikoa ya Lindi, Pwani, Mtwara na Ruvuma, Mrajisi wa Ushirika, viongozi wa vyama vikuu vya ushirika wa Korosho katika kikao kilichojadili  upatikanaji wa pembejeo za  zao hilo kwenye  ukumbi wa Mkuu wa mkoani wa Lindi.

 Pia, Waziri Mkuu ameitaka bodi hiyo isimamie mwenendo wa ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa vya kubangulia korosho katika maeneo yote yanayolima zao hilo ili kuondokana na uuzwaji wa korosho ghafi.

Amesema lazima bodi hiyo ambayo ameizindua  iwajibike ipasavyo katika kuhakikisha inaongeza uzalishaji wa zao hilo na iwapo itashindwa Serikali haitosita kuivunja. 

 “Lazima mfuatilie na kuufahamu mwenendo wa zao mnalolisimamia na mjue mfumo unaotumika katika mauzo yake. Pia muwe na takwimu za wakulima na ukubwa wa mashamba yao ili kuweza kuwahudumia kwa urahisi,”

 Pia ameitaka bodi hiyo iweke mkakati wa utoaji wa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na faida ya kulima zao la korosho kwa kutumia magari maalumu, kuwafuata  maeneo walipo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema tayari mchakato wa kuviwezesha vyama vya wakulima kuanza ubanguaji wa korosho umeanza ambapo katika msimu wa mwaka huu TANECU imepata mkopo kutoka CRDB na itaanza kubangua tani 2,500.

Amesema vyama vingine vitakavyofuata utaratibu huo baada ya TANECU ni TAMCU, MAMCU na RUNALI ambavyo vyote vinampango wa kuanzisha viwanda vyenye uwezo wa kuchakata tani 2,5000 za korosho kwa mwaka.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile, amesema wamepokea maelekezo na maagizo yote kwamba watayafanyia kazi kwa kusirikiana na wajumbe wa bodi hiyo na menejimenti na hawatafanyakazi kwa mazoea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles