23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

TAMWA yawaonya wanahabari wachanga

Na Ashura Kazinja, Morogoro

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Dkt Rose Reuben, amewashauri waandishi wa habari wachanga nchini kujiweka mbali na ukatili wa kingono ndani ya vyombo vya vyao ili kukomesha vitendo hivyo.

Rose ametoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitano ya Dar es salaam, Mwanza, Morogoro, Dodoma, na Singida juu ya ukatili wa kingono ndani ya vyumba vya habari yaliyoandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la kusaidia vyombo vya habari (IMS), yaliyofanyika mkoani hapa.

Mkurugenzi huyo amesema kutokana na mdahalo uliofanyika juzi mkoani hapa wa kuangalia wingi wa matendo ya ukatili wa kingono kwenye vyumba vya habari, wanahabari walionekana kuwa nafasi ya 11 kati ya kura 21 zilizopigwa kutoka kwa wanahabari ambao kati yao wanaume walikuwa 4 ikitofautishwa na wahariri na wamiliki waliopata kura 13.

“Mwanahabari mchanga anayetoka chuoni akiingia kwenye chumba cha habari na kukubali kufanyiwa ukatili wa kingono lazima ataendeleza matendo hayo pale atakapopata nafasi ya kuwa mhariri, hali hiyo haitaisha” amesema.

Amesema wingi wa changamoto hiyo kwa wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kushika nafasi ya 13 ni chachu ya kuonesha kuwa changamoto hiyo inaanzia chini kwa wanahabari wenyewe.

Katibu wa Klabu ya Waandishi mkoa wa Morogoro (Moro- PC) Lilian Lucas, ameiomba Serikali kutambua kuwa ni wakati muafaka umefika wa serikali kusaidia na kuondoa suala la ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya habari nchini.

Amesema kupitia mdahalo uliofanyika wa wanahabari umewasaidia kujifunza mengi na kwamba watakuwa mstari wa mbele wa kufichua masuala ya ukatili wa kijinsia yanayowakumba na kuiambia Serikali kwa uwazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles