23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wahasibu watakiwa kuacha udokozi

Brighiter Masaki

Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo, amekiomba Chama cha Wahasibu na wadau wake kuzingatia weledi  na kuacha udokozi katika utendaji kazi pamoja na kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato katika Sekta za umma na binafsi.

Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania, Mkumbo, amesema uboreshaji wa mfumo wa mapato utaendelea kuisaidia serikali katika kutekeleza miradi.

“Uboreshaji wa mfumo wa mapato utaendelea kuisaidia serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa nchi ya kipato cha juu zaidi.”

“Nafasi ya taaluma ya uhasibu inaongozwa na dira ya Taifa letu katika kutengeneza dira, kuwafanya wananchi kuwa na maisha bora na kusababisha nchi yetu kuwa na utawala bora na uchumi imara.” amesema  Mkumbo.

Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Wahasibu Tanzania, Cpa Peter  Mwambuja, amesema kuwa wanashukuru serikali kuheshimu taaluma ya wahasibu kwa kutambua mchango wao.

Amesema cha hicho kinasaidia kutengeneza mabilionea wengi zaidi kupitia wahasibu.

“Tutaonyesha  fadhira kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa wahasibu wazuri zaidi,  makini na kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu, kumbuka tulikuwa na sheria za wahasibu zilitusaidia wahasibu kutambulika kwa kusajiliwa na kuendelea na kazi”

Aidha chama hicho kilitoa  tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya biadhara kidato cha sita ambao kwa sasa wapo vyuo tofauti tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles