25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu aagiza mradi wa umeme JNHPP kukamilika kwa wakati

MWANDISHI WETU-RUFIJI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115 na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Tito Mwinuka ausimamie ili ukamilike kwa wakati.

Vilevile, Waziri Mkuu amemwagiza mkandarasi anayejenga mradi huo aukamilishe kwa wakati kwa sababu imebainika kuwa mvua zinazoendelea kunyesha nchini haziathiri utekelezaji wake.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana akiwa katika ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kuwa ameridhishwa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, kazi inayofanyika ni ya uhakika huku kukiwa na matumaini makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa,” alisema Majaliwa.

Mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unajengwa na Kampuni ya Arab Construction kwa pamoja na Kampuni ya Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri.

Unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya taifa na kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Mbali na kuliwezesha taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kupungua kwa changamoto ya ajira baada ya Watanzania wengi wakiwemo wakandarasi kupata ajira za kudumu na za muda mfupi.

Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles