30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WHO: Huenda virusi vya Corona vikabakia kama HIV

GENEVA, USWISI

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, huenda virusi vya Corona visiishe bali vikabakia milele na kuwa kama ilivyo kwa virusi vya Ukimwi (HIV).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango ya Dharura wa WHO, Dk. Mike Ryan, ambaye ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.

Ofisa huyo wa ngazi za juu wa WHO alieleza kwamba, “ni muhimu kufahamu kwamba, virusi vya corona vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na virusi hivi huenda visiishe”. 

Alitanabahisha kwa kusema kuwa, huenda virusi hivi vikawa kama vile vya HIV ambavyo kimsingi havijaisha lakini watu sasa wamevizoea.

Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zinazofanyiwa utafiti, lakini Dk. Ryan alisema kwamba, kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.

Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona, na karibu watu milioni 4.5 wameshaambukizwa virusi hivyo katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Marekani ndio yenye maambukizo na idadi kubwa ya vifo vya ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na virusi vya corona ambapo hadi sasa karibu watu milioni na nusu wameambukizwa virusi hivyo huku zaidi ya 85,000 wakiaga dunia nchini humo.

Hispania, Urusi, Uingereza na Italia zinafuata kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ya virusi vya corona.

Barani Afrika nchi ya Afrika Kusini ndio yenye maambukizo mengi baada ya kurekodi kesi 12,074, ikifuatiwa na Misri ambayo iimethibitisha kesi 10,431 za maambukizo ya corona.

Algeria na Morocco zinafuata katika orodha hiyo. Katika Ukanda wa Afrika Mashariki takwimu zinaonyesha kuwa, Kenya imeathiriwa zaidi na virusi vya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles