23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wanawake TACAIDS waadhimisha siku ya Wanawake Duniani

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Watumishi wanawake kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wameungana na Wizara na  sekta binasi pamoja Taasisi nyingine nchini kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya  Siku ya wanawake Duniani kilichofanyika katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma tarehe 8Machi2023.

Maadhimisho hayo yaliongozwa na kauli mbiu isemayo Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia, ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.

Watumishi wanawake wa TACAIDS wakiwa katika maandamano wakati wa maadhimisho ya
Kilele cha Siku ya wanawake Duniani Machi 8, 2023.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Machi 8, mwaka huu, Senyamule alisesema lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutaka kuhamasisha jamii juu ya uwezo wa wanawake katika kuleta Usawa wa Kijinsia na maendeleo ya kiuchumi, na kuisistiza kuwepo kwa usawa wa kijinsia mahala pa kazi hususan katika shughuli zote za maendeleo ikiwemo nafasi za maamuzi, siasa na umiliki wa mali pamoja Ardhi.

Aliongeza kuwa wanawake ni Jeshi kubwa wakiwezeshwa wanaweza na wamesisitizwa kuepuka vishawishi vya kuingia kwenye ndoa za jinsia moja.

Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TACAIDS, Magreth Mrema akizungumza baada ya maandamano alisema mshikamano kwa wanawake ni jambo la msingi ikiwa ni pamoja na kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia kuanzia katika familia ,jamii   kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles