23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania kuwa mwenyeji maonyesho ya LPG

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afriks Mashariki litakalofanyika Machi 15 na 16, mwaka huu katika hoteli ya Johari Lotans Dar es Salaam likihusisha nchi zaidi ya 30.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mapema Machi 9, 2023 Mkurugenzi wa Maonyesho ya LPG Afrika Mashariki(East Afrika LPG Exp, Catherine Ho amesema kuwa, Tanzania inawawezesha wajumbe kukutana na watu mashuhuri katika sekta ya LPG, wakiwemo viongozi wa biashara, Vyama vya Kimataifa, Maofisa wa Serikali na watendaji wa C-Suite.

Amesema lengo la kongamano hilo ambalo linadhaminiwa na kampuni ya Oryx Energies na Sygma Cylinders ni kuandaa mikakati ya kukabiliana na changamoto za sasa na kutumia maarifa ya wasomi yanayoweza kuamua soko la kesho.

“Tumebaini kuwa kuna ongezeko kubwa la matumizi ya LPG nchini Tanzania, hivyo kupitia maonyesho haya yatasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza idadi kubwa ya matumizi ya nishati safi,” amesema Catherine

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wadau wanaohusika na biashara ya gesi ya kupikia majumbani (LPG), Amos Jackson amesema tukio hilo ni la muhimu na litawezesha kuelewa namna gani dunia nzima inashughulika na gesi ya kupikia majumbani.

“Ni vizuri wadau wote wapate nafasi ya kusikiliza na tuweze kushirikiana kukuza biashara ya gesi Tanzania,” amesema Jackson.

Aidha, amesema kuwa katika kongamano hilo kutakuwa na Wawakilishi kutoka nje ya nchi ambao ni watengenezaji wa vifaa mbalimbali vinavyotumika katika biashara ya gesi, kutakua na waelimishaji watakaolezea manufaa ya gesi ambayo imetoka duniani kote.

“Mwaka jana kulikua na mkutano wa kuhamasisha watu kutumia gesi au nishati safi zaidi kuliko nishati ambazo tunazitumia sasahivi za kuni na mkaa, ambapo rais alizungimzia namna gani nchi yetu inataka kuelekea katika muelekeo wa kupunguza Matumizi ya nishati safi na hii inaendana na lengo la umoja wa mataifa ya kuimarisha uchumi na kuinua maisha ya watu wanaoishi katika umaskini ambapo katika lengo namba 7 linalenga kuhakikisha kila mtu anapata nishati safi kwaajili ya kutunza afya yake na kutunza mazingira,” amesema Jackson.

Aliongezea kuwa kampuni za gesi zimejitahidi kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ili gesi isiwe bei kubwa lakini serikalini kwa upande wake imefanya kazi kubwa kwa kuondoa kodi kwa upande wa gesi.

Jackson ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika biashara ya gesi ya kupikia majumbani na kupelekea kuongeza wawekezaji wengi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles