27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

DC Ileje akemea ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

Na Denis Sikonde, Songwe

WAKATI wanawake wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wakiadhimisha siku ya wanawake duniani imeelezwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2022 na 2023 jumla ya wanawake 357 na watoto 54 wamebakwa ndani ya mwaka mmoja.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Machi 6, 2023 katika kijiji cha Ikumbilo kata ya Chitete wilayani humo.

Mgomi amesema takwimu za watoto kufanyiwa ukatili kwa Ileje ndani ya mwaka imekuwa ya kutisha licha ya wengine kutobainika jamii inatakiwa ishirikiane lielimishe ili watoto waepushwe na magonjwa ya kuambukizwa, mimba za utotoni na kulawitiwa kwa watoto wa kiume.

“Watoto 55 ni wengi sana na wilaya ya Ileje siyo mkoa, jamani ni aibu sana na huenda kuna wengine ambao wamefanyiwa ukatili hawajabainika niwaombe tulipoti kwenye vyombo husika ikiwemo ustawi wa jamii na dawati la jinsia,” amesema Mgomi.

Amesema jamii inapaswa kuelimisha watoto kutambua namna wanavyoweza kufanyiwa ukatili na kuwambia wapi wanapaswa kulipoti ili wahusika wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi akitoa msaada kwa wazee.

“Sisi wazazi na walezi tutenge muda kuzungumza na watoto kujua maendeleo yao na kuwapa ujasiri wa kukataa na kukemea kwani wasipofanya hivyo wataharibiwa ndoto zao,” amesema Mgomi.

Akisoma risala kwenye maadhimisho hayo, Lucy Mwani kutoka ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Ileje kitengo cha maendeleo ya jamii amesema katika kesi 357, kesi 17 wanawake walipigwa na waume zao, na wanawake 340 wenye watoto walitelekezwa na waume zao.

Katika hatua nyingine Mwani amesema katika kipindi hiki halmashauri kupitia Ustawi wa Jamii imepokea jumla ya matukio 55 ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto kubakwa hali ambayo jamii inapaswa kushirikiana kupiga vita.

Akizungumza katika maadhimisho hayo baada ya kugawiwa taulo za kike, Sifa Leonard mwanafunzi wa shule ya wasichana Ileje amesema kushamili kwa ukatili dhidi ya watoto Kunatokana na baadhi ya watoto kukosa elimu ya malezi na nanna ya kukabiliana na vishawishi, hivyo msaada huo utawasaidia kutokosa vipindi vya masomo darasani na kujiepusha na vishawishi.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikumbilo, Joseph Lwinga amesema wanapaswa kujiepusha na mila kandamizi zinazopelekea ukatili dhidi ya watoto sambamba na mila potofu za kuwabaka watoto ili tujenge kizazi na familia bora ya baadaye.

Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zilizofanyika ni pamoja na kutoa mikopo kwenye vikundi vitatu vya wanawake kutoka asilimia 4 kati ya asilimia 10 kutoka mapato ya ndani, kugawa taulo Kwa wanafunzi ya wasichana Ileje ,na kugawa mahitaji Kwa baadhi ya wazee wasiojiweza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles