26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Watu 50 wahofiwa kupoteza maisha mgodini Congo

KINSHASA, CONGO

TAKRIBANI watu 50 wengi wao wakiwa ni vijana wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa dhahabu karibu na eneo la Kamituga Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, shirika moja lisilo la kiserikali katika eneo hilo limesema.

Tukio hilo limetokea baada ya kunyeesha mvua kubwa katika eneo la Kamitunga lililoko Kivu Kusini.

“Wachimbaji kadhaa walikuwa kwenye shimo la mgodi ambalo lilifunikwa na udongo na hakuna mtu aliyeweza kuokolewa. 

Inadaiwa vijana 50 ndio walikuwa katika shimo hilo la mgodi” amesema Emiliane Itongwa, kiongozi wa shirika moja la wanawake.

Visa vya watu kufukiwa migodini hutokea mara nyingi katika nchi mbalimbali duniani, na watu wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na hali hiyo.

Jamhuri ya Kidemekrasia ya Congo ni nchi tajiri kwa dhahabu, almasi na coltan lakini migodi mingi inadhibitiwa na makundi yenye silaha.

Watu wa DRC ni miongoni mwa watu maskini zaidi barani Afrika ingawa nchi hiyo ni tajiri kwa rasilimali.

Mashariki mwa Congo  kumekuwa na migogoro kwa karibu miaka 24 sasa, huku jeshi na makundi ya waasi yakituhumiwa kutumia mapigano kama kisingizio wakati vikichota utajiri wa madini katika eneo hilo.

Wachambuzi wanasema soko la kimataifa kwa madini ya Coltan ni mojawapo ya vyanzo vya mgogoro na kuwepo kwa wanamgambo nchini humo.

Mwezi Mei 2011 serikali iliondoa kizuizi kwenye machimbo ya mashariki, eneo lililoathiriwa zaidi na migogoro ya DRC ya muda mrefu.

Makampuni ya kigeni ndio wawekezaji wakubwa nchini DRC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles