26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jimbo Nigeria lapitisha sheria ya kuhasi wabakaji

KADUNA, NIGERIA

KUMEKUWA na maandamano na ghadhabu nchini Nigeria miezi ya hivi karibuni kutokana na ongezeko la vitendo vya ubakaji.

Kutokana na hali hiyo Wabunge katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria wamepitisha adhabu ya kuwahasi wale wataokutwa na hatia ya kuwabaka watoto walio chini ya umri wa miaka minne.

Gavana wa jimbo hilo, Nasir Ahmad el-Rufai anatakiwa kutia saini muswada huo ili kuwa sheria katika jimbo hilo la Kaskazini Magharibi.

Awali aliunga kono adhabu hiyo ili kudhibiti vitendo vya ubakaji kujirudia.

Sheria nchini Nigeria inaelekeaza adhabu ya kifungo cha miaka 14 na kifungo cha maisha, lakini wabunge wanaweza kuweka adhabu ya tofauti.

Unyanyapaa huwafaya waathirika kushindwa kuripoti matukio ya ubakaji nchini Nigeria na idadi ya watu waliofikishwa kwenye vyombo vya sheria ni ndogo.

Mnamo mwezi Juni magavana wa Nigeria walitangaza hali ya hatari kutokana na matukio ya ubakaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Tangu mwaka 2015, wakati sheria mpya ilipoanzishwa, watuhumiwa 40 wa ubakaji wameshtakiwa, kulingana na Wakala wa Kitaifa wa kuzuia usafirishaji haramu wa watu (NAPTIP), ambayo ina orodha ya wahalifu wa udhalilishaji wa kijinsia kwenye tovuti yake.

Sheria hiyo mpya iliongeza wigo ambao makosa ya unyanyasaji wa kijinsia yanaweza kuadhibiwa nchini Nigeria na kuondoa ukomo wa muda wa miezi miwili wakati kesi za ubakaji zilipaswa kuhukumiwa kabla ya muda wa mwisho kusikilizwa kortini.

Mkuu wa shirika hilo, Julie Okah-Donli, ameiambia BBC kuwa changamoto ya kesi hizi ni kuthibitisha kesi ya ubakaji .

‘Itawadhibiti wabakaji’

Kuwatoa nguvu za kiume wabakaji waliopatikana na hatia umepigwa marufuku nchini Nigeria kwa muda, hasa wakati matukio haya yameongezeka wakati wa marufuku ya kutotoka nje kutokana na janga la virusi vya corona.

Kulikuwa na ghadhabu kubwa mwezi Julai baada ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 ambaye familia yake inasema alibakwa kisha akauawa.

Ilikuwa moja ya matukio kadhaa ya kushangaza ndani ya wiki moja ambayo ilisababisha maandamano ya mitaani, yaliyoungwa mkono na maelfu ya watu na kampeni ya mtandaoni ya Twitter isemayo #WeAreTired. (Tumechoka)

uwavera Omozuwa alibakwa na kuuawa mwezi Julai katika mji wa Kusini mwa Nigeria, Benin.

Raia wengi wa Nigeria wametaka kuwepo kwa adhabu kali, kama vile hukumu ya kifo.

”Tunafikiri sheria mpya itasaidia sana kuondokana na idadi ya matukio yanayoongezeka ya ubakaji kwenye jio letu,” alisema mbunge wa Kaduna Shehu Yunusa alipozungumza na BBC.

”Ikiwa gavana wa Kaduna atatia saini muswada huu kuwa sheria, mbakaji mwingine atakayekamatwa Kaduna atakuwa mtu wa kwanza kuhasiwa chini ya sheria mpya,” alisema .

Mwanaharakati wa masuala ya jinsia Dorothy Njemanze, ambaye pia ni alikuwa muathirika wa ubakaji ameunga mkono muswada huu akionesha shauku yake kwa majimbo mengine kuiga mfano wa Kaduna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles