26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa kuongoza tamasha la kumpongeza JPM

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la “karibu Dodoma “linalotarajiwa kufanyika Oktoba 22-24 jijini hapa.

Lengo la tamasha hilo ni kupongeza juhudi za Rais John Magufuli katika kukuza na kutangaza Dodoma kuwa ni Jiji, ikiwa ni sehemu za kuendeleza fikra za baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  juu ya makao makuu kuhamia Dodoma.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na mratibu wa tamasha hilo, ambaye ni Msanii wa Bongo Muvi, Saimon Mwapagata maarufu kwa jina la Rado wakati akizungumza na waandishi wa habari .

Mwapagata alisema tamasha hilo litakuwa na maudhui ya kutoa fursa kwa makundi mbalimbali ya jamii na kwenye sekta mbalimbali ambazo zimefanya vizuri na kuleta mabadiliko  chanya kwa jamii.

“Tunatumia Jiji la Dodoma katika kuratibu mambo makubwa yanayo unganisha taifa kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi,”alisema.

Alisema katika kutoa fursa ilivyokusudiwa makundi ya jamii pamoja na sekta mbalimbali zitapewa nafasi ya kutoa ushihuda wa mabadiliko yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa  Dk. Jonh Magufuli.

“Tunapaswa kutoa shukrani zetu kwa Serikali ya awamu ya tano, na katika kufanya hivyo kuna baadhi ya makundi yaliyopata mabadiliko ya ushindi ndani ya miaka makundi hayo yatapata nafasi ya kueleza ushindi huo.

“Makundi hayo ni pamoja na bodaboda, mama ntilie, machinga, watu wenye ulemavu, wanafunzi wa vyuo, vijana, wanawake na wazee,”alisema.

Alisema tamasha hilo halipo kisiasa na kwamba wananchi wanapaswa kutofautisha tamasha hilo na nguvu ya siasa .

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu Tanzania, John Mlabu alisema, kundi hilo linatambua mchango wa Serikali ya awamu ya tano hivyo kwa nguvu moja wameamua kuunga mkono tamasha hilo.

“Tunashuhudia Rais akiwajali walemavu kwa vitendo, jamii ilizoea kuona walemavu wakiwa ombaomba, maisha yao yalikuwa magumu, lakini sasa hali imebadilika tuna nafasi ya kufanya biashara na kujijenga kiuchumi,”alifafanua.

Naye, Mwakilishi wa wanawake wajasiriamali wa Dodoma, Mariam Fentu alieleza kuwa ni wakati wa kuyaweka hadharani mambo waliyifanyiwa na Serikali ya Magufuli ambapo alisema imewashika mkono kwa asilimia 99.

“Tulimkopesha Magufuli kura zetu na Sasa anatulipa maendeleo kwa vitendo,tunafanya biashara kwa mikopo nafuu ya asilimia 4 iliyotolewa na Serikali kwa kundi la wanawake”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles