31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 37 wahukumiwa kifo nchini Misri

 CAIRO, MISRI

MAHAKAMA moja nchini Misri imewahukumu adhabu ya kifo watu 37 akiwemo Hisham al Ashmawy, Ofisa wa zamani wa jeshi la nchi hiyo aliyejiunga na magenge ya kigaidi.

Ashmawy alitiwa mbaroni katika mji wa Derna wa mashariki mwa Libya mwishoni mwa mwaka 2018 na alikabidhiwa kwa maofisa wa Misri mwezi Mei mwaka jana. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Ashmawy alipatikana na hatia ya makosa mengi ikiwemo kufanya njama za shambulio lililotokea mwaka 2014 na kuua wanajeshi 22 wa Misri karibu na mpaka wa Libya na pia kuhusika katika jaribio la kumuua waziri wa mambo ya ndani wa Misri mwaka 2013.

Ofisa huyo wa zamani wa jeshi la Misri alikuwa anaongoza kundi linalojiita Ansar Bayt al Maqdis ambalo ni moja ya makundi hatari nchini Misri na ambalo mwaka 2014 lilitangaza utiifu wake kwa genge la kigaidi la Daesh yaani ISIS.

Watu wengine 36 waliohukumiwa kifo pamoja na Ashmawy, nao walipatikana na hatia ya makosa ya ugaidi.

Hukumu za watu hao amekabidhiwa Mufti Mkuu wa Misri ambaye kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, hukumu za kifo hupelekwa kwake kwanza kupata maoni yake kabla ya kutekelezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles