28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ufilipino yaripoti kifo cha kwanza cha corona

 MANILA, UFILIPINO

UFILIPINO imeripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi vipya vya Corona nje ya China ambapo Serikali ya China imechelewesha kufunguliwa kwa shule katika mkoa ulioathirika zaidi wa Wuhan nchini humo.

Pia imeimarisha hatua za kimatibabu katika mji ambao unaruhusu mtu mmoja pekee kutoka kununua bidhaa za matumizi.

Idara ya afya nchini Ufilipino, ilisema kuwa mwanamume mmoja raia wa China wa umri wa miaka 44 kutoka Wuhan, alilazwa Januari 25 baada ya kupata joto kali na kukohoa. 

Baadaye aligunduliwa kuwa na homa ya mapafu na baada ya matibabu hali yake ikaimarika. 

Hata hivyo saa 24 kabla ya kifo chake, hali yake iligeuka kuwa mbaya zaidi na kufariki baada ya kugunduliwa kuwa na virusi hivyo vya Corona. 

Mwenzake wa kike wa umri wa miaka 38 pia kutoka Wuhan, amethibitishwa kuwa na virusi hivyo na ametengwa ili kupata matibabu katika hospitali moja mjini Manilla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles