29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WATU 30 WAUAWA UCHAGUZINI PAKISTAN

 

BALUCHISTAN, PAKISTAN


WATU 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye kituo kimoja cha kupigia kura katika jimbo la Baluchistan jana wakati mamilioni ya Wapakistan wakiwa katika vituo vtya kupigaa kura.

Kwa mujibu wa afisa mmoja kwenye mji wa Quetta ulio kusini magharibi mwa Pakistan, Hashim Ghilzai, mshambuliaji aliyejifunga mabomu alikuwa akijaribu kujipenyeza kwenye kituo cha kupigia kura, ndipo alipojiripua na kuua watu 30 akiwamo yeye mwenyewe.

Dk. Muhammad Jaffar wa Hospitali ya Sandeman walikopelekwa baadhi ya maiti na majeruhi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa miongoni mwa waliouawa ni watoto wa miaka minane na sita.

“Hadi sasa tumepokea miili 21, akiwemo msichana wa miaka minane na mvulana wa miaka sita”, alisema daktari huyo.

Kupitia shirika lake rasmi la habari, Amaq, kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS) lilidai kuhusika na mashambulizi haya, yakiwa ya karibuni zaidi katika jimbo masikini kabisa la Baluchistan, ambalo limekuwa kiini cha makundi kadhaa ya uasi na siasa kali.

Serikali imesambaza wanajeshi 370,000 na askari polisi 450,000 nchi nzima kusimamia ulinzi kwenye uchaguzi huu wa jana.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa mwisho wa maoni, si yeyote kati ya nyota wa kriketi aliyegeuka mwanasiasa, Imran Khan, na waziri mkuu wa zamani aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa ufisadi, Nawaz Sharif, anayeweza kupata ushindi wa moja kwa moja.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles