24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 100 WAFA NJAA NDANI YA SAA NANE SOMALIA

MOGADISHU, SOMALIA


WAZIRI Mkuu wa Somalia, Hassan ali Khaire, amesema watu 110 wamefariki dunia kutokana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hii katika kipindi cha saa nane tu.

Ukame mbaya unaoikumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini hapa.

Tangazo hilo la Khaire linakuja siku chache baada ya Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, kutangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.

Umoja wa Mataifa (UN) una kadiria watu milioni tano nchini Somalia wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza taifa hili ni moja kati ya manneyaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.

Mataifa mengine ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.

Karibu watu 260,000 walifariki nchini hapa kutokana na baa la njaa kuanzia mwaka 2010 na 2012 huku wengine 220,000 wakiwa wamefariki kwa sababu hiyo hiyo mwaka 1992.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles