30.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

WATOTO WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA AJILI YA BODABODA

 

Na TAUSI SALUM, DODOMA


WATU wanne wakiwamo watoto watatu wa familia, wamefariki dunia papohapo baada pikipiki maarufu kama (bodaboda), waliyokuwa wamepanda kugongana na basi la abiria.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni Yusra Salum (5), Karialino Hamis (2), Husein Hamisi (miezi miwili) na Mfaume Hamis (30) ambaye ni dreva wa bodaboda.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema ajali hiyo ilitokea juzi usiku wilayani Bahi mkoani Dodoma katika barabara kuu ya Singida-Dodoma.

Alisema mwendesha pikipiki huyo alikuwa amewapakia watoto watatu na mama yao kisha kuingia kwenye barabara hiyo ghafla ambapo aligongwa na basi la kampuni ya SATCO.

Kamanda Muroto alieleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.

“Kwenye hiyo pikipiki walikuwa wamepanda jumla watu watano, watoto watatu na mama yao, dereva, watoto na dreva walifariki dunia papohapo, mama wa hawa watoto amelazwa hospitali akitibiwa majeraha aliyopata,”alisema Kamanda Muroto.

Alisema ajali zinapoteza nguvu kazi na kuwaasa vijana wanaoendesha pikipiki kuwa makini kwenye matumizi ya barabara.

“Bodaboda ni miongoni mwa matatizo, tunawaasa mzingatie sheria za barabarani, kila kitu mnakiona rahisi, katikati ya magari mnapita, mtapoteza maisha yenu na Serikali itapoteza nguvu kazi,”alisema.

Muroto aliwataka kuzingatia sheria za usalama barabarani na wananchi waendelee kushirikiana na jeshi la polisi.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles