24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEDAIWA KUTAKA KUMUHONGA LUKUVI SH MILIONI 90 KIZIMBANI

 

NA KULWA MZEE – DAR ES SALAAM


MKURUGENZI wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Co. Ltd, Mohamed Kiluwa, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Kiluwa alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kupandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akimsomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru, Maghela Ndimbo, alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 16, mwaka huu, kati ya saa 6.10 na saa nane mchana, katika ofisi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, iliyoko wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Inadaiwa mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Kiluwa Steal Group Co. Ltd na Kiluwa Free Processing Zone, alitoa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 (sawa na Sh milioni 90) kwa Waziri Lukuvi kama kishawishi ili asimtake awasilishe wizarani hapo hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 kitalu ‘B’ Kikongo na kitalu ‘D’ kwenye eneo la viwanda Disunyura, lililoko Kibaha Mjini, jambo ambalo linaendana na shughuli za kazi za Lukuvi.

Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Imani Madega, alikana shtaka hilo, huku upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilka.

Pia Wakili Ndimbo alidai hawana pingamizi kuhusu dhamana na kuiomba mahakama kuzingatia matakwa ya sheria wakati inatoa masharti ya dhamana.

Kwa upande wake, Madega aliomba mahakama kumpatia mteja wake dhamana kwa masharti yaliyoelekezwa na sheria.

Hakimu Mashauri alitoa masharti ya dhamana yaliyomtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho, ambao mmoja kati yao awasilishe mahakamani fedha taslimu Sh milioni 45 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho.

Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi imepangwa kwa kutajwa Agosti 15, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles