23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

WATOTO WAKATIWA BIMA YA AFYA

Dorocella Reuben
Dorocella Reuben

Na CLARA MATIMO- MWANZA

WATOTO 45 wamekatiwa bima ya afya na Shirika la Foundation Dart linalosaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi watoto hao bima hizo katika kituo cha afya Buzuruga jana, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dorocella Reuben, alisema hiyo ni zawadi muhimu kwa walengwa kwa kuwa sasa watakuwa na uhakika wa matibabu endapo wataugua.

Alisema tangu shirika hilo lianzishwe mwaka 2012, limekuwa likitoa misaada mbalimbali kwa watoto wa kike ambao wanaishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kielimu kwa kuwanunulia vifaa vya shule, kuwalipia ada na mafunzo ya ufundi, lakini wanapougua huingia gharama kubwa kwa ajili ya kuwapatia matibabu.

“Tulikaa na viongozi wenzangu tukatafakari tukaona ni bora tuwakatie bima watoto wetu hawa ili wawe na uhakika wa matibabu, tumeanza na hawa wachache lakini tutaendelea kuwakatia wengine kadiri Mungu atakavyotuwezesha, naomba Watanzania wenzangu wenye uwezo wawatafute watoto ambao familia zao hazijiwezi wawakatie bima.

“Tumeamua kuwakabidhi leo hizi bima zao ikiwa tunaelekea katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpaya kama sehemu ya zawadi za shirika kwao, maana hakuna zawadi kubwa kama ya uhai, unapokuwa na bima una uhakika wa kuokoa maisha,” alisema.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga, Dk. Masoud Masele, alipongeza shirika hilo kwa kuwakatia watoto hao bima hizo za afya zenye thamani ya Sh 180,000. Alisema hivi sasa watakuwa na uhakika wa kupata matibabu katika hospitali zilizo ndani ya Manispaa ya Ilemela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles