25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

TAASISI YA BENJAMIN MKAPA YATOA MAJENGO YA SH BILIONI 1.9

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Na SAMWEL MWANGA- SIMIYU

TAASISI ya Benjamin Mkapa, imekabidhi majengo mawili ya upasuaji na nyumba 28 kwa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya watumishi wa idara ya afya zote zikiwa na thamani ya Sh bilioni 1.9.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika maeneo tofauti ya mkoa huu ambapo majengo mawili ya upasuaji yalikabidhiwa katika Kituo cha Afya Ngulyati katika Halmashauri ya mji wa Bariadi.

Pia sehemu ya nyumba hizo zilikabidhiwa katika Hospitali ya Mkula katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega ambapo  zilipokelewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Akisoma taarifa kwa Ummy, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Dk. Ellen Senkoro, alisema wakati taasisi hiyo inaadhimisha miaka 10  ya kazi zao  wamechangia  jitihada mbalimbali za Serikali hapa nchini  ikiwemo katika Mkoa wa Simiyu.

Alisema taasisi hiyo imekuwa ikitekeleza  miradi mbalimbali kuanzia mwaka 2011 hadi 2016, ambayo imelenga kuimarisha  mfumo wa sekta ya afya.

Alisema Taasisi hiyo mpaka sasa imejenga  nyumba 480 kati ya nyumba hizo, 48 zipo katika Mkoa wa Simiyu wilaya za Busega (10), Bariadi (8), Itilima (10) Maswa (10) na Meatu (10), lakini hadi sasa tayari nyumba 28 nyingine zilikabidhiwa juzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles