26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto 800,000 kupewa chanjo ya polio awamu ya nne Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Desemba Mosi, 2022 Mkoa wa Simiyu unaanza zoezi la kutoa chanjo ya matone ya Polio kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano, ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa Desemba 04, 2022.

Katibu tawala Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo akizungumza Novemba 30, mwaka huu kwenye kikao cha kamati ya Afya msingi ya Mkoa, amesema kuwa chanjo hiyo ni mwendelezo wa chanjo nyingine zilizotolewa katika awamu ya kwanza, ya pili na tatu.

Amesema kuwa katika awamu ya nne, mkoa unarajia kutoa chanjo kwa watoto wapatao 869, 040, ambapo amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanahasisha jamii kujitokeza kwa wingi kwenye kampeini hiyo.

Katibu tawala huyo amesema kuwa katika awamu zilizopita, mkoa umefanya vizuri zaidi kwa kufikia malengo yake, ambapo katika awamu ya tatu mkoa ulifikia asilimia 115.7 ikiwa ni zaidi ya lengo lake.

Mratibu wa Chanjo Mkoa Beatrice Kapufi ameeleza kuwa katika awamu ya nne, chanjo itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya serikali na binafsi ikiwa pamoja na uwepo huduma maalum ya mkoba.

“Tutakuwa pia na huduma maalumu ya mkoa (Mobile Clinick) ambapo huduma hiyo itafanyika kwenye maeneo au vijiji ambavyo havina huduma za Afya, lakini pia chanjo itatolewa pia kwenye ofisi za vijiji, vitongoji na kata,” amesema Kapufi.

Mratibu huyo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha malengo wanayafikia na kuzidi zaidi kama ambavyo walifanya awamu ya tatu, huku akiwataka wazazi na walezi kuwaleta watoto wao wenye umri wa kupata chanjo hiyo.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa, Dk. Yahaya Nawanda amewataka viongozi wa Dini kutumia nyumba za Ibada kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo ya Polio awamu ya nne inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Pia Dkt. Nawanda amewaagiza viongozi wengine kuanzia ngazi ya kaya, Vitongoji, Vijiji, Mitaa, kata na Wilaya kuwa mabalozi na wahamasishaji wa zoezi la chanjo ili liweze kufanikiwa na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Aidha amesema kuwa mkoa umejipanga kutoa chanjo zote kwa watoto wanaohitajika huku akijihakikishia kuwa zoezi hilo litatekelzwa kwa asilimia 100 na kuwasisitiza watendaji wa Idara ya afya kujipanga kwa ajili ya kufikia malengo makubwa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles