22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

TBL yazindua mfumo wa ukusanyaji taarifa za ajali za barabani nchini

Na Mohammed Ulongo, Mtanzania Digital

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imezindua mfumo wa Usalama barabarani utakaowezesha jeshi la polisi kukusanya taarifa za ajali barabarani  kupitia simu janja zitakazoweza kupunguza ajali barabarani.

Mfumo huo mpya wa Usalama barabarani utaliwezesha jeshi hilo kupitia askari wa usalama barabarani kukusanya taarifa ama vyanzo vya ajali na mapendekezo ya ushahidi, ambayo yataongoza mipango ya maendeleo na kuhamasisha juhudi za kuboresha usalama barabarani pamoja ili kuokoa maisha ya watanzania.

Ajali za barabarani zimekuwa changamoto kubwa hivyo kuzinduliwa kwa mfumo huwo kutasaidia kupunguza ajali hizo na kuwajengea uelewa askari wa usalama kwa kuwapa elemu ya matumizi ya vifaa vya kielekroniki katika kutimiza majukumu yao.

Hata hivyo, imebainishwa kuwa mfumo huo ni wa majaribio hivyo utaanza kutumika Dar es Salaam pekee hadi hapo baadae utakapowezeshwa utatumika nchi nzima.

Mfumo huo wa usalama barabarani ni wa kwanza na ni wa aina yake, hivyo utaendelea kupimwa na kuboreshwa kupitia maoni mbalimbali kutoka kwa polisi wa barabarani ambao ndio wanufaika wakubwa wa mfumo huo hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wamekuwa ni wahanga wakubwa wa ajali za barabarani hivyo anaishukuru kampuni ya TBL kufanikisha uzinduzi huo.

“Kipekee niwashukuru TBL kwa kuweza kusaidia kudhibiti na kupunguza ajali za bodaboda kwa kutenga bajeti maalum kwani bodaboda wamekuwa ni wahanga wa ajali za barabarani kwani ipo haja kwa kundi hili kulifanya kuwa salama ili wasije pata madhara yatokanayo na ajali za barabarani,” amesema Kamanda Ng’anzi na kuongeza kuwa:

“Pia niwashukuru kwa kuwajengea uzoefu askari wetu na maofisa kwani sisi ndiyo wasimamizi wa sheria barabara hivyo kufanya hivyo kunawezesha kupunguza ajali kwani sasa kuna mabadiliko kama ya njia ya Kimara hadi Kibaha kutoka njia sita na hadi nane hivyo ni jambo jema pamoja na kutoa elimu kwa waendesha vyombo vya moto hasa bodaboda,”.

Kamanda Ng’anzi amehitimisha kwa kuiahidi kampuni ya TBL kushirikiana vyema na kuitumia ipasavyo katika ukusanyaji wa taarifa za usalama wa barabarani kutumia mfumo huwo mpya ili kutokomeza ajali barabrani nchini.

Nae Mkurugenzi wa Usambazaji TBL, Nancy Riwa amesema: “TBL inajivunia kwa uzinduzi wa mfumo huu wa usalama barabarani, na ni hatua nyingine ambayo tumechukua kuboresha usalama nchini Tanzania, kwani usalama wa barabarani ni muhimu kwenye kila nyanja ya maisha yetu ya kila siku na ni muhimu kujenga miji endelevu na jamii iliyo salama,” amesema Nancy.

Aidha, Mkurugenzi huyo ameongezea kwa kusema kuwa na kupitia mfumo wa UNITAR wamefanikiwa kutoa mafunzo kutumia zana za kiusalama ambapo mafunzo hayo yaliwapa nafasi maofisa hawa kujua kwa undani matumizi ya zana hizo ikiwa ni sehemu ya kuboresha miundombinu ya usalama barabarani.

Kukamilika kwa mfumo huo ni sehemu ya ahadi iliyowekwa na Kampuni ya TBL ikiwa na lengo la kusaidia mipango ya serikali, ambayo ni pamoja na kutoa elimu juu ya utumiaji mbaya wa pombe, kuendelea kusimamia sera bora, kuendeleza mipango inayoashiria ushirikiano mzuri na wadau wake. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles