29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

WATATU KIZIMBANI KWA DAWA ZA KULEVYA

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


WATU watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya heroine na valium.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Ramadhan Mkimbo, aliieleza mahakama kuwa katika shtaka la kwanza, mshtakiwa Nassoro Issah Februari 16, mwaka huu huko Magomeni Kagera alitenda kosa hilo kinyume cha sheria.

Alidai, Nassoro alikamatwa na kete 20 za heroine gramu 1.3 na dawa aina ya valium gramu 7.2, alizokuwa akiwauzia watuhumiwa wenzake.

Katika shtaka jingine, watuhumiwa Fadhili Said na Nuru Daud,  walipandishwa kizimbani wakikabiliwa na kosa la kutumia dawa za kulevya, wakifahamu kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Watuhumiwa wote walikana kuhusika na makosa hayo na mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika na kuiomba kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa shtaka hilo.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Frank Moshi, alisema dhamana iko wazi kwa washtakiwa wote na kuwataka kupeleka wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja.

Washtakiwa wote walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Aprili 11, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles