24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

WATANZANIA HAWAKIDHI KIWANGO CHA ULAJI NYAMA

Na ELIYA MBONEA

Kiwango cha ulaji nyama kwa Mtanzania mmoja kimetajwa kuwa cha chini zaidi kwa mwaka ikilinganishwa na viwango vinavyopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Katika kipindi cha Mwaka 2012/ 13 na Mwaka 2016/17 ulaji wa nyama kwa kila Mtanzania umeendelea kuwa kilo 12 kwa mwaka badala ya kilo 50 zinazopendekekezwa na wataalamu duniani.

Aidha katika kipindi cha Mwaka 2015/16 takwimu zimeonyesha kuwa ulaji wa nyama kwa kila Mtanzania uliweza kuongezeka kidogo na kufikia angalau kilo 15 kwa mwaka.

Ofisa Usajili Mifugo kutoka Bodi ya nyama Tanzania, Ezekiel Maro amesema tatizo hilo la ulaji nyama kwa Watanzania linachangiwa na gharama za mifugo husika.

Maro amesema kuwapo kwa gharama hizo kumesababisha gharama za uzalishaji kuwa juu na hivyo kuwafanya walaji wa nyama nchini kuhamia katika matumizi ya mboga nyingine.

“Lakini pia ukosefu wa elimu nao ukiwa ni sehemu ya tatizo linalowafanya watu kushindwa kula nyama kwani baadhi yao hawajui faida zake, tunahitaji kuongeza elimu na kiwango cha uzalishaji nyama ili wananchi waanze kula nyama kwa wingi,” amesema.

Hata hivyo, amesema baadhi ya sababu zilizosababisha kushuka kwa uzalishaji wa nyama nchini kuwa ni pamoja na uhaba wa vyakula vya mifugo kama mbuzi, kondoo, kuku na nguruwe.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles