23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MASHINE ZA EFD IRINGA UTATA MTUPU

NA FRANCIS GODWIN

Mashine za kielektroniki (EFD), zimezua kizaa zaa mkoani Iringa baada ya baadhi ya vinyozi na mama lishe wenye migahawa maeneo ya Miyomboni ya Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA), kuwafungia   biashara zao kwa kutokuwa na mashine hizo za kutolea risiti.

Zoezi hilo limefanyika wiki mbili zilizopita katika msako wa biashara zisizo na mashine hiyo ambapo baadhi ya wafanyabiashara waliofungiwa wamelalamikia hatua hiyo kutokana na kipato kidogo wanachopata kupitia biashara hizo.

Mfanyabiashara wa chakula eneo la Miyomboni, Michael Simon amesema TRA ilifunga mgahawa  wake kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kuuza  chakula bila ya kutoa risiti za EFD ila kwa  sasa amelazimika kununua mashine hiyo.

Amesema biashara anayofanya haina tofauti na ile  ya mama lishe isipokuwa eneo limewaponza kutokana na bei ya pango katika maeneo hayo.

Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Ramson Tulianje  amesema vinyozi na wafanyabiashara ambao  wanapaswa kuwa na mashine ni wale ambao kwa  siku wanauza kati ya Sh 40,000 na kuendelea bila  kujali anafanya shughuli gani.

“Eneo  hilo la Miyomboni bei ya kupanga vyumba  ni Sh 400,000 kwa mwezi, hivyo kwa kodi hiyo  anatambuliwa kama mfanyabiashara mkubwa  hawezi kuuza  sawa na mfanyabiashara aliyepo nje ya mji,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles