26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Watalii kutoka nje ya nchi kushuhudia kupatwa jua Mbeya

MakalaNa Pendo Fundisha, Mbeya

WAGENI mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wameanza kuwasili mkoani hapa kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali.

Tukio hilo la historia ambalo kwa mara ya mwisho linatajwa na wataalamu kwamba lilitokea mwaka 1977, linatarajia kutokea tena Septemba mosi mwaka huu nchini Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza.

Akizungumzia tukio hilo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, alisema   Serikali imeanza kupokea wageni mbalimbali kutoka ndani ya nchi na nje.

“Baadhi ya wageni  kutoka nje ya nchi ambao wamewasili tayari ni kutoka Ujerumani, wengine watawasili leo kutoka Zambia na Malawi, lakini wageni wa ndani ni wengi,” alisema.

Alisema  kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu, inasemekana tukio la kupatwa kwa jua litatokea katika maeneo mawili tofauti katika  mikoa miwili ya Nyanda za Juu Kusini.

Alisema  mkoani Mbeya, tukio hilo litatokea Rujewa wilayani Mbarali  na   mkoani Njombe ni katika eneo la Wanging’ombe.

“Maeneo yote mawili inasemekana jua litapatwa kwa asilimia 90 na tayari vifaa mbalimbali vimeshawasili ikiwamo miwani maalum ambayo itatumika kuangalia jua wakati likipatwa,” alisema.

Makalla  amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia kifaa maalumu kutazama jua linavyopatwa kuepuka madhara ya macho.

Hata hivyo, Makalla alisema mkoa umejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwa wa uhakika wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles