25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Watakiwa kuepuka magonjwa ya mlipuko

Timothy Itembe  Mara

JAMII mkoani Mara imetakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu,  corona na mengine katika kipindi cha kuelekea  kumaliza  mwaka 2020 ili kujenga taifa lenya watu wa afya na maendeleo.

Mganga Mkuu wa mkoa Mara, Florian Tinuga, karibuni alisema magonjwa kama hayo yanakwamisha maendeleo na rasilimali fedha pindi yanapokuwa yamepokuwa yanawakumba wanajamii huku yakidhoaafisha nguvu kazi.

Tinuga aliwataka waandishi kuendelea kutoa elimu ya madhara ya magonjwa yamlipuko kwa jamii na jamii kuendelea kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kama vile corona huku wakizingatia usafi wa mazingira katika maeneo husika.

Mganga huyo aliwatoa hofu Watanzania juu ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kuwa sasa haupo licha ya kuwa upo katika mataifa mengine na kuwa kuna haja ya kuchukua tahadhari.

“Tanzania kupitia jitihada za Rais John Magufuli hatuna ugonjwa wa corona licha ya kuwa mataifa mangine bado ugonjwa huu upo kwa hali hiyo jamii inatakiwa kuchukua tahadhari,”alisema Tunuga.

Kwa upande wa mwenyekiti wa clabu ya waandishi wa habari mkoa  Mara, Rabsoni Wangaso, alitumia nafasi hiyo kuwahimiza awaandishi wahabari kutoa elimya ya madhara ya magonjwa ya mlipuko kwa kutumia kalamu zao.

Wangaso aliongeza kusema kutokana na kutolewa elimu jamii inaendelea kubadilika na kuchukua tahadhari inayotolewa ya magonjwa ya mlipuko kupitia  wizara husika ili kujenga taifa la watu na maendeleo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles