30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yaanzisha bustani kuvutia mji Geita

NA MWANDISHI WETU-GEITA

WAKAZI wa Mji wa Geita wanafurahia kuwa sehemu ya mradi wa bustani ya kupumzikia inayofadhiliwa  na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Geita. 

Mradi huo uliotengewa bajeti ya Sh milioni 70 kutoka fedha za mfuko wa GGML za uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) zinatarajiwa kukamilisha mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua ujenzi wa bustani hiyo katika kata ya Kalangalala mjini Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema GGML kwa kushirikiana na Halmashauri ya Geita Mji inatekeleza mradi huo kupitia fedha za Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutoka GGML.

Alisema mradi huo unaotekelezwa katika eneo la mita za mraba 4000 katika kata ya Kalangalala mjini Geita, una lengo la kuwapatia wakazi wa Mji wa Geita fursa ya kuwa na eneo la kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kupumzika, kupunga upepo pamoja na kuepuka kero za joto.

“Lengo letu ni kuona wakazi wa Mji wa Geita wanafika katika eneo hili kufurahia upepo asilia sanjari na kuona mnara maalum wenye kumbukumbu ya Mkoa wa Geita.

“Bustani hii itakuwa kivutio pia kwa vile inajengwa kwa tofali za kuvutia kwenye maeneo yote ya kupitia na sehemu za watu kuketi hali ambayo itashawishi watu wengi zaidi kukaa na kujionea uzuri wa Mji wetu wa Geita,”alisema RC Gabrile 

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema kuwa Kampuni ya GGML imekuwa ikifanya jitihada kubwa kubadilisha muonekano wa jamii ya Mkoa wa Geita kwa kuanzisha miradi endelevu. 

“GGML tunajivunia kuwa, wakati tunasherehekea miaka 20 ya uwekezaji wetu ndani ya Mkoa wa Geita mwaka huu, tumefanikiwa kutekeleza miradi mingi yenye tija na matokeo chanya ikiwemo mnara wa makutano ya barabara Mjini Geita, masoko, taa za barabarani, vituo vya afya, shule na barabara za lami,” alisema Richard Jordinson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles