27.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Watainiwa masomo ya dini ya kiislamu darasa la saba waongezeka

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

JOPO la Wataalam wa Elimu ya Kiislamu Tanzania (IEP), limesema idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani wa masomo ya dini ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu kwa wanafunzi wa darasa la saba limeongezeka kutoka 150,945 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 157,823 kwa mwaka huu.

Mtihani huo ulifanyika Agosti 9 mwaka huu,pamoja na mtihani wa kuhitimu madrasa uliofanyika Agosti 12 na 13, mwaka huu.

Akizungumza leo Agosti 23, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mjumbe jopo la IEP, Alhaji Sheikh Musa Kundecha amesema jumla ya shule 3,975 katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwa vya Unguja na Pemba walifanya mtihani huo huku halmashauri 159 zilishiriki kufanya mtihani huo.

Amesema idadi ya shule zilizofanya mtihani huo umeongezeka kutoka 3903 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 3975 sawa na asilimia 1.8 kwa mwaka huu.

“Hivi sasa idadi imeongezeka tofauti na mwaka jana hiyo imetokana na ongezeko la kuwepo kwa shule katika halmashauri,” amesema Alhaj Sheikh Kundecha.

Amesema, idadi ya Halmashauri zilizoshiriki katika mtihani huo imeongezeka kutoka halmashauri 151 hadi kufikia halmashauri 158 kwa mwaka huu.

Amesema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa somo la elimu ya dini ya Kiislamu walikuwa 174,719 kati ya hao waliofanya walikuwa 157,823 sawa na asilimia 90.33.

Sheikh Alhaji Kundecha amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata daraja A hadi D ni 139,181 sawa na asilimia 88.19 sawa na idadi ya watahiniwa wote .

Ametaja shule kumi bora zilizopo katika halmashauri ambazo Temeke, Nachingwea, Mkuranga, Mwnza, Ilemela, Dodoma, Mafia, Kigamboni, Bukoba na Masasi.

Sheikh Alhajj ametaja shule kumi za mwisho katika mtihani huo zimetoka katika halmashauri za Tabora, Same, Urambo, Kisarawe, Kilimanjaro na Mpanda.

Aidh,a ameeleza kuwa lengo ni kuratibu madrasa zote ziwepo kwenye mfumo zilizopo mtaani na madrasa zinapata changamoto wa mwingiliano wa mitihani ya shule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles