25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Juhudi za Rais Samia zachochea Tanzania kuwa mwenyeji Jukwaa la Mifumo ya Chakula

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa jukwaa la mifumo ya chakula (AGRF) litakalofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 5, mpaka 8, mwaka huu ikiwa ni juhudi zilizofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassani kuboresha sekta ya kilimo na kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo.

Akizungumzia Agosti 23, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano huo Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini Wizara ya Kilimo, Joseph Kiraiya amesema ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huo umekuwa wa tofauti na miaka ya nyuma kwani mwanzo ilikuwa kwa kuchaguliwa lakini sasa wenyeji wa mkutano huo imetokana na kushindanishwa na nchi nyingine.

“Mafanikio tunayoyaona sasa katika wizara ya kilimo ni kutokana na jitahada zinazofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu katika sekta ya kilimo hivyo ni mapinduzi makubwa yaliyofanyika yanatoa matokeo chanya Kwa taifa,” amesema Kiraiya.

Amesema kuwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula itatoa fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo hivyo taasisi na sekta binafsi zinapaswa kujisajili ili kushiriki katika katika mkutano huo ambao unatarajiwa kushirikisha maraisi na wakuu wa nchi mbalimbali duniani.

Amesema matarajio ya mkutano huo ni kukuza sekta ya utalii kwani kutakua na utalii wa kilimo ambapo wageni watatembelea maeneo mbalimbali ili kujionea uzalishaji unaofanywa nchini.

Aidha, Kiraiya ameongeza kuwa mkutano huo utaongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi kwa Taifa lakini pia kukuza biashara na kuhamasisha uwekezaji.

“Mageuzi ya sekta ya kilimo yataletwa na vijana na wanawake hivyo jukwaa hili ni fursa Kwa Kila mmoja wetu kuitumia ili kukuza kipato na kuinua uchumi wa nchi yetu,” ameongeza.

Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wakuu wa nchi ambapo mpaka sasa wizara ya kilimo imetoa mialiko kwa Marais 17 na mawaziri wanohusika na maswala ya kilimo na uvuvi 43 lakini washiriki waliojisajili mpaka sasa ni 2,300 huku lengo likiwa kuwa na washiriki 3,000.

Akizungumzia kuhusu maandalizi Kiraiya amesema kuwa mpaka Sasa maandalizi yote muhimu yameshakamilika ikiwemo maeneo watakayofikia wageni pamoja na sehemu za vivutio watakavuotembelea.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Septemba 5 hadi 8, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles